Mafungo ya siku 40

Ninakukaribisha kushiriki pamoja nasi Mafungo ya siku 40.

Mafungo haya ni maalumu kwaajili ya kumshukuru Mungu kwa kumaliza mwaka wa 2024 lakini pia tutakua na mafundisho na maombi maalumu ya kuombea malengo na mipango ya mwaka unaokuja wa 2025

Rev. Dr. Eliona Kimaro nitaongoza na kufundisha katika mafungo haya. Pia nitafundisha Neno kuu litakalotuongoza kwa Mwaka unaokuja wa 2025.

Mafungo yataanza Jumatatu ya tarehe 4 November mpaka 13 December. Vipindi vyetu vitakuwa ni asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi na jioni kuanzia saa 1 kamili Usiku
Na Mungu wetu wa mbinguni atakuhudumia kwa ajili ya utukufu wa Jina lake. Jitahidi sana usikose!!

Mungu akubariki sana.